2 Corinthians 11:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi — nanena hayo kiwazimu — ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, wao ni watumishi wa Al-Masihi? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii zaidi yao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimepigwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, wanamtumikia Kristo? Mimi ninamtumikia zaidi sana. (Je, mimi ni mwendawazimu kuongea kwa jinsi hii?) Nimefanya kazi kwa juhudi kuliko wao. Nimekuwa gerezani mara nyingi. Nimepigwa vibaya sana. Nimekuwa katika hali za hatari ya kufa mara nyingi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi—nanena hayo kiwazimu—ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi — nanena hayo kiwazimu — ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, wao ni watumishi wa Kristo? Nanena kiwazimu, mimi ni zaidi yao: Nimefanya kazi kwa bidii kuliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, nimekabiliwa na mauti mara nyingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, wao ni watumishi wa Al-Masihi? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii kuwaliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi – nanena hayo kiwazimu – ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni watumishi wa Kristo? Mimi nawapita; nasema kama mwenye wazimu. Nimesumbuka kuwapita, nimefungwa kuwapita, nimepigwa kuwapita kabisa, mara nyingi nimetakiwa kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa nitasema kama mwenda-wazimu: wao ni watumishi wa Kristo? Mimi ni mutumishi wake zaidi kuliko wao. Nimetumika kazi nyingi zaidi, nimefungwa mara nyingi zaidi, nimepigwa zaidi, na mara nyingi nimekuwa katika hatari ya kufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wao wakhudumu wa Kristo? (nanena kiwazimu), mimi zaidi; kwa kazi kuzidi sana; kwa mapigo kupita kiasi; kwa vifungo kuzidi sana; kwa mauti marra nyingi.