2 Corinthians 11:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipigwa fimbo mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tatu nilipigwa mijeledi, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nilivunjikiwa na meli, nilikaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara tatu katika nyakati tofauti nimepigwa kwa fimbo. Mara moja nilikuwa karibu kuuawa kwa kupigwa kwa mawe. Mara tatu nimevunjikiwa na merikebu, na mara moja katika hizo nilikesha usiku na kushinda kutwa nzima tukielea baharini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilipigwa viboko mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipigwa fimbo mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tatu nalichapwa kwa fimbo, mara moja nalipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tatu nilichapwa kwa fimbo, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara tatu nilipigwa kwa bakora; mara moja nilipigwa kwa mawe; mara tatu nilivunjikiwa jahazi; kutwa kucha nimepata kukaa kilindini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipigwa fimbo mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mara tatu nalipigwa viboko, mara moja nalipigwa mawe, mara tatu chombo changu kimevunjika baharini, nikawamo kilindini usiku na mchana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waroma wamenipiga fimbo mara tatu na mara moja walitaka kuniua kwa kunitupia mawe. Mara tatu chombo nilichosafiri nacho kilizama kwa kuvunjika. Mara moja, nilishinda ndani ya bahari kwa muda wa siku nzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra tatu nalipigwa bakora; marra moja nalipigwa mawe; marra tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;