2 Corinthians 11:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi; nimejua kukaa njaa na kuona kiu; nimefunga kula chakula mara nyingi; nimehisi baridi na kuwa uchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimefanya kazi ngumu na za kuchosha, na mara nyingi sikuweza kulala usingizi. Nimekuwa mwenye njaa na kiu. Mara nyingi nimekosa kula chakula. Nimekuwa katika hali ya baridi na kutokuwa na nguo za kujifunika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi, ninajua kukaa njaa na kuona kiu, nimekaa mara nyingi bila chakula, nimesikia baridi na kuwa uchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi; ninajua kukaa njaa na kuona kiu; nimefunga kula chakula mara nyingi; nimehisi baridi na kuwa uchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimeumia, mpaka nikachoka, nikikesheshwa mara nyingi, nikiumizwa na njaa na kiu, nikinyimwa mara nyingi vyakula, nikiwekwa penye baridi pasipo nguo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimesumbuka kwa kufanya kazi ngumu, nimepata magumu, nimekesha mara nyingi. Mara nyingi niliteswa na njaa na kiu; mara nyingi nililazimishwa kutokula. Nimeteseka na baridi na ukosefu wa nguo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kazi na kusumbuka; kwa kukesha marra nyingi; kwa njaa na kiu; kwa kufunga marra nyingi; kwa baridi na kuwa uchi.