2 Corinthians 11:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, ni nani aliye mdhaifu, nami nisijisikie mdhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninajisikia kuwa mdhaifu kila mara mtu mwingine anapokuwa dhaifu. Ninapata hasira sana pale mtu yeyote anapoingizwa dhambini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, ni nani aliye dhaifu, nami nisijisikie dhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, ni nani aliye mdhaifu, nami nisijisikie mdhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko mnyonge asiyenitia unyonge nami? Yuko anayekwazwa, nisipoumizwa nami?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kukiwa mutu anayepatwa na uzaifu, mimi ninajisikia muzaifu vilevile. Kukiwa mutu anayeanguka katika zambi, ninasikia uchungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu na mimi? Nani aliyechukizwa na mimi nisiwake?