2 Corinthians 11:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ila nina hofu kuwa nia zenu zitapotoshwa muache kujitoa kwa dhati na kumfuata Yesu Kristo kwa moyo safi. Hili laweza kutokea kama vile Hawa alivyodanganywa na nyoka kwa akili zake za ujanja wenye udanganyifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama nyoka alivyomdanganya Ewa kwa werevu wake mbaya, ninao woga wa kwamba: Vivyo hivyo nayo mawazo yenu yataangamizwa, msiweze tena kuandamana na Kristo peke yake tu na kumng'alia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninaogopa kwamba sawa vile nyoka alivyomudanganya Eva kwa werevu wake, mawazo yenu vilevile yasipotoshwe hata mupate kupoteza uaminifu na ukamilifu wenu kwa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.