2 Corinthians 11:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, nyinyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au Injili tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu mtu akija na kuwahubiria Isa mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnaonekana kuwa na subira na mtu yeyote anayekuja kwenu na kuwaeleza habari za Yesu aliye tofauti na Yesu yule ambaye sisi tuliwaambia habari zake. Mnaonekana kuwa radhi kuipokea roho au ujumbe ulio tofauti na roho na ujumbe ambao mlioupokea kutoka kwetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, ninyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au habari njema tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, nyinyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au Injili tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Isa mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au Injili nyingine msiyoikubali, mnavumiliana naye punde!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, nyinyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au Injili tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtu anapokuja kwenu na kutangaza Yesu mwingine, tusiyemtangaza sisi, au mnapopata roho nyingine, msiyoipata, au mnapotangaziwa Utume mwema mwingine, msioupokea, basi, ninyi huvumilia vizuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii inatokana na kuona jinsi munavyomukubali mutu yeyote anayekuja kwenu na kuwahubiri habari za Yesu mwingine asiyekuwa yule sisi tuliyemuhubiri. Na zaidi ya hii munakubali upesi kupokea roho ingine na ujumbe mwingine vinavyokuwa tofauti na Roho au Habari Njema muliyopokea toka kwetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana yeye ajae akikhubiri Yesu mwingine ambae sisi hatukumkhubiri, au mkipokea Roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumilia nae.