2 Corinthians 11:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilifanya kazi ya kutangaza Habari Njema za Mungu kwenu bila malipo. Nilijinyenyekeza ili kuwafanya ninyi kuwa wa muhimu. Je! Mwadhani nilikosea katika hilo?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekeza ili nipate kuwakweza ninyi. Je, nilifanya vibaya?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Nilifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu niliwahubiria Injili ya Mungu bila ujira?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekesha ili nipate kuwakweza nyinyi. Je, nilifanya vibaya?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au nimekosa, nilipojinyenyekeza, ninyi mpate kuwa wakubwa? Au nimekosa, kwa kuwa nimewatangazia Utume mwema wa Mungu pasipo malipo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi niliwatangazia Habari Njema ya Mungu bila kudai mushahara. Nilijinyenyekeza kusudi mupate kutukuzwa. Basi kwa kujinyenyekeza vile, nilifanya kosa?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Je! nalifanya dhambi kwa kujinyenyekea illi ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwakhubiri Injili ya Kristo bila ujira?