2 Corinthians 11:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliyanyang’anya makundi mengine ya waumini kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naliwanyang'anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipokea malipo toka makanisa mengine. Ilikuwa kana kwamba nimechukua fedha toka kwao ili niweze kuwatumikia ninyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Niliyanyang'anya makanisa mengine kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliyanyang’anya makundi mengine ya waumini kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Niliwanyang'anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho yangu ili niwahudumie ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wateule wengine nimewapokonya na kutwaa matunzo, nipate kuwatumikia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naliwanyang’anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipokuwa nikitumika kati yenu nililipwa na makanisa mengine. Ni kama vile nilinyanganya mali ya makanisa yale na kuitumia kwa kuwasaidia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Naliwanyangʼanya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu niwakhudumie ninyi.