2 Corinthians 11:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nilipopungukiwa na chochote, sikuwa mzigo kwa mtu yeyote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walitimiza mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yoyote, nami nitaendelea kujizuia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama nilihitaji chochote nilipokuwa nanyi, sikumsumbua yeyote kati yenu. Kina kaka waliofika kutoka Makedonia walinipa yote niliyohitaji. Sikutaka kuwa mzigo kwenu kwa namna yeyote ile. Na kamwe sitakuwa mzigo kwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nikipungukiwa na cho chote, sikuwa mzigo kwa mtu ye yote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walinipatia mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yo yote, nami nitaendelea kujizuia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nikipungukiwa na chochote, sikuwa mzigo kwa mtu yeyote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walinipatia mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yoyote, nami nitaendelea kujizuia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo, nilipokuwako kwenu, nikawa nimekosa vyakula, hakuna, niliyemsumbua. Kwani ndugu waliokuja toka Makedonia waliniongezea, nilivyovikosa. Katika mambo yote nimejiangalia, nikae kwenu pasipo kuwasumbua, navyo ndivyo, nitakavyojiangalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati nilipokuwa kwenu, sikumulemea mutu yeyote nilipohitaji kitu fulani, kwa maana wandugu waliotoka Makedonia waliniletea vitu vyote nilivyohitaji. Nilijiangalia vizuri katika mambo yote kusudi nisiwalemee, nami nitaendelea kujiangalia vema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda.