2 Corinthians 12:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimekuwa kama mpumbavu, lakini nyinyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Nyinyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimejifanya mjinga, lakini mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora”, ingawa mimi si kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nimekuwa nikizungumza kama mjinga, lakini ninyi ndiyo mliosababisha nikafanya hivyo. Ninyi ndiyo mnaopaswa kuzungumza mema juu yangu. Mimi si kitu, lakini mimi si myonge kwa njia yeyote ile kwa hao “mitume wakuu”.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimekuwa kama mpumbavu, lakini, ninyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Ninyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo zaidi kuliko hao “mitume wakuu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimekuwa kama mpumbavu, lakini nyinyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Nyinyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekuwa mjinga, lakini ninyi mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora,” ingawa mimi si kitu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekuwa mjinga, lakini ninyi mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora,” ingawa mimi si kitu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimekuwa kama mpumbavu, lakini nyinyi mmenilazimisha kuwa hivyo. Nyinyi ndio mngalipaswa kunisifu. Maana, ingawa mimi si kitu, kwa vyovyote, mimi si mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimekuwa mpuzi wa kujivuna, lakini ninyi mmenishurutisha. Kwani ingefaa, mimi nisifiwe nanyi. Kwani hakuna, nishindwacho nao wale wajipao macheo yote ya utume, hata nikiwa si kitu mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninasema kama mupumbafu, lakini ni ninyi ndio mumenilazimisha kufanya vile. Kufuatana na ile, ningepaswa kusifiwa nanyi. Kwa maana hata kama mimi si kitu, wale mitume wenu wanaohesabiwa kuwa wakubwa hawanipiti kitu kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu, nijapokuwa si kitu.