2 Corinthians 12:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, mlipungukiwa nini zaidi kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu kwamba mimi kwa upande wangu sikuwasumbueni kupata msaada wenu? Samahani kwa kuwakoseeni haki hiyo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, ninyi ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makundi mengine ya waumini, ila tu kwamba mimi sikuwa mzigo kwenu? Nisameheni kwa kosa hili!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo mlipokea kila kitu ambacho makanisa yote yalipata. Kitu kimoja tu ndicho kilikuwa cha tofauti na cha kipekee: Sikuwa mzigo au msumbufu kwenu. Mnisamehe kwa hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, mlipungukiwa nini zaidi kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu kwamba mimi kwa upande wangu sikuwasumbueni kupata msaada wenu? Samahani kwa kuwakoseeni haki hiyo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, mlipungukiwa nini zaidi kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu kwamba mimi kwa upande wangu sikuwasumbueni kupata msaada wenu? Samahani kwa kuwakoseeni haki hiyo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, ninyi ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila tu kwamba mimi sikuwa mzigo kwenu? Nisameheni kwa kosa hili!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, ninyi ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makundi mengine ya waumini, ila tu kwamba mimi sikuwa mzigo kwenu? Nisameheni kwa kosa hili!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe kosa hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, mlipungukiwa nini zaidi kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu kwamba mimi kwa upande wangu sikuwasumbueni kupata msaada wenu? Samahani kwa kuwakoseeni haki hiyo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kuna nini, mliyopungukiwa kuliko wateule wengine, isipokuwa hii tu, ya kuwa sikuzila mali zenu ninyi? Niachilieni upotovu huu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumepungukiwa na nini kuliko makanisa mengine, isipokuwa tu kwamba mimi sikuwalemea kwa kupata musaada toka kwenu? Munisamehe kwa kosa hili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, illa kwa kuwa mimi sikuwalemea. Mnisamehe udhalimu huo.