2 Corinthians 12:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni nyinyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Nami sitawalemea, kwa sababu sihitaji chochote chenu, ila ninawahitaji ninyi. Kwa kuwa watoto hawaweki akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi huweka akiba kwa ajili ya watoto wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Niko tayari sasa kuwatembelea kwa mara ya tatu, na sitakuwa mzigo kwenu. Mimi sitafuti kitu chochote kilicho chenu. Ninawataka ninyi tu. Watoto wasiweke akiba vitu vya kuwapa wazazi wao. Wazazi wanapaswa kuweka akiba vitu vya kuwapa watoto wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni ninyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni nyinyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa niko tayari kuja kwenu kwa mara hii ya tatu, nami sitawalemea, kwa sababu sitahitaji cho chote chenu, ila ninawahitaji ninyi, kwa kuwa hata hivyo watoto hawaweki akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi huweka akiba kwa ajili ya watoto wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa niko tayari kuja kwenu kwa mara hii ya tatu, nami sitawalemea, kwa sababu sitahitaji chochote chenu, ila ninawahitaji ninyi, kwa kuwa hata hivyo watoto hawaweki akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi huweka akiba kwa ajili ya watoto wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa niko tayari kabisa kuja kwenu mara ya tatu, na sitawasumbua. Maana ninachotafuta si mali zenu, bali ni nyinyi wenyewe. Ni kawaida ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba, na si watoto kuwawekea wazazi wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, mara hii ni ya tatu, nikiwa tayari kuja kwenu, tena sitazila mali zenu. Kwani siyatafuti yaliyo yenu, ila nawatafuta ninyi wenyewe. Kwani haifai, watoto wawawekee wazazi wao vilimbiko, ila wazazi sharti wao wawawekee watoto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa mimi niko tayari kufika kwenu kwa mara ya tatu, nami sitawalemea. Maana sihitaji mali yenu, lakini ninawahitaji ninyi. Kwa sababu si kazi ya watoto kuwawekea wazazi wao akiba, lakini ni kazi ya wazazi kuwawekea watoto wao akiba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tazama hii ni marra ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawidemea. Maana sitafuti vitu vyenu, bali ninyi: maana haiwapasi watoto kuwawekea akiba wazazi, bali wazazi watoto.