2 Corinthians 12:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda nyinyi mno?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Je, ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo ninayo furaha kutumia kile nilichonacho kwa ajili yenu. Na mimi mwenyewe nitajitoa kikamilifu kwa ajili yenu. Je, kama upendo wangu kwenu utakuwa mkubwa, upendo wenu kwangu utapungua?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda ninyi mno?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda nyinyi mno?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Hata ingawa inaonekana ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Hata ingawa inaonekana ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitakuwa radhi kutumia na kutumiwa kwa ajili yenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi ni radhi kabisa kutumia nilicho nacho, na hata kujitolea mimi mwenyewe kabisa, kwa faida ya roho zenu. Je, mtanipenda kidogo ati kwa kuwa mimi nawapenda nyinyi mno?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi yanipendezayo sana ni kutoa yaliyo yangu, kweli hata mwenyewe nitatolewa kwa ajili yenu ninyi; nikijipingia kuwapenda, itafaa nikipungukiwa kupendwa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ngambo yangu, nitafurahi kutumia vyote ninavyokuwa navyo na kujitoa mimi mwenyewe, kwa ajili yenu. Ikiwa ninawapenda zaidi namna hii, hamupaswi kupungukiwa na upendo kwangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu: ingawa nizidipo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?