2 Corinthians 12:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu mwingine atasema: “Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Iwe iwavyo, kwa vyovyote vile, mimi sikuwalemea. Lakini wengine wanadhani mimi ni mjanja, nami niliwapata kwa hila!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni wazi kuwa sikuwa mzigo kwenu, lakini baadhi yenu wanadhani kuwa nilikuwa mjanja, na kutumia hila kuwaweka mtegoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu mwingine atasema: “Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu mwingine atasema: “Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iwe iwavyo, kwa vyo vyote vile mimi sikuwalemea. Lakini kwa mimi kuwa mwerevu naliwapata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Iwe iwavyo, kwa vyovyote vile mimi sikuwalemea. Lakini kwa mimi kuwa mwerevu naliwapata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu niliwapata kwa hila.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mtakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu. Lakini labda mtu mwingine atasema: “Kwa vile Paulo ni mwerevu, amewafanyieni ulaghai.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, kwa sababu mimi sikuwasumbua, wale husema: Kwa kuwa mwenye werevu mbaya nimewakamata kwa hila.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mutakubali kwamba mimi sikuwalemea. Lakini watu wengine wanafikiri kwamba mimi ni mwerevu na nimewanasa kwa kuwadanganya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.