2 Corinthians 12:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Labda mnafikiri kwamba mpaka sasa tumekuwa tukijitetea wenyewe mbele yenu! Lakini, tunasema mambo haya mbele ya Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo. Mambo hayo yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili ya kuwajenga nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, mmekuwa mkifikiri kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu? Sisi tumekuwa tukinena mbele za Mungu kama wale walio katika Al-Masihi. Na chochote tufanyacho, ndugu wapendwa, ni kwa ajili ya kuwatia nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je! Mnadhani tumekuwa tukijitetea? Hapana, tunasema haya katika Kristo na mbele za Mungu. Ninyi ni rafiki zetu wapendwa, na kila tunachofanya tunakifanya ili muwe imara.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Labda mnafikiri kwamba mpaka sasa tumekuwa tukijitetea wenyewe mbele yenu! Lakini, tunasema mambo haya mbele ya Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo. Mambo hayo, yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Labda mnafikiri kwamba mpaka sasa tumekuwa tukijitetea wenyewe mbele yenu! Lakini, tunasema mambo haya mbele ya Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo. Mambo hayo yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili ya kuwajenga nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, mmekuwa mkifikiri kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu? Sisi tumekuwa tukinena mbele za Mungu kama wale walio katika Kristo na cho chote tufanyacho, ndugu wapendwa ni kwa ajili ya kuwatia nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, mmekuwa mkifikiri kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu? Sisi tumekuwa tukinena mbele za Mungu kama wale walio katika Al-Masihi. Na chochote tufanyacho, ndugu wapendwa, ni kwa ajili ya kuwatia nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mnadhani hata sasa ya kuwa najitetea kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Labda mnafikiri kwamba mpaka sasa tumekuwa tukijitetea wenyewe mbele yenu! Lakini, tunasema mambo haya mbele ya Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo. Mambo hayo yote, wapenzi wangu, ni kwa ajili ya kuwajenga nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmeanza kale kutuwazia, ya kuwa twajikania mbele yenu. Lakini Mungu ajua: twasema kwa kuwa wake Kristo. Nayo yote tunayasema, tuwajenge ninyi, wapenzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi munazani kwamba kwa wakati huu wote sisi tunajitetea mbele yenu? Tunasema mambo yale mbele ya Mungu kufuatana na vile tunavyoungana na Kristo. Wandugu wapendwa, mambo yale yote ni kwa kuwajenga ninyi katika imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwadhani ya kuwa tunajindhuru kwenu tena? Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na haya yote, wapenzi, kwa ajili ya kuwajenga.