2 Corinthians 12:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Namjua mtu mmoja katika Al-Masihi ambaye miaka kumi na nne iliyopita alichukuliwa juu hadi mbingu ya tatu. Kama ni katika mwili au nje ya mwili, sijui, Mungu ajua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninamjua mtu mmoja katika Kristo aliyechukuliwa juu katika mbingu ya tatu. Hili lilitokea miaka 14 iliyopita. Sifahamu ikiwa mtu huyu alikuwa ndani ya mwili wake au nje ya mwili wake, lakini Mungu anajua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alichukuliwa juu hadi mbingu ya tatu. Kama ni katika mwili au nje ya mwili, sijui, Mungu ajua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Namjua mtu mmoja katika Al-Masihi ambaye miaka kumi na minne iliyopita alichukuliwa juu hadi mbingu ya tatu. Kama ni katika mwili au nje ya mwili, sijui, Mwenyezi Mungu ajua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko mtu nimjuaye kuwa mwenye Kristo; sasa miaka yapata 14, kama alikuwa mwilini, sijui, au kama alikuwa ametengwa na mwili wake, sijui; Mungu anayajua. Mtu huyo alipokonywa na kupelekwa, mpaka aiingie mbingu ya tatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninamujua mutu mumoja aliyeungana na Kristo, na sasa kumekwisha kupita miaka kumi na mine, mutu huyu akanyanyuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Ikiwa alinyanyuliwa katika hali ya kimwili au ya kiroho mimi sijui, Mungu peke yake anajua.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Namjua mtu mmoja katika Kristo, impita sasa miaka arobatashara, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui, Mungu ajua). Mtu huyu alichukuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.