2 Corinthians 12:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyo, kunongona, majivuno na fujo kati yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninafanya hivi kwa sababu ninaogopa kuwa nitakapokuja, hamtakuwa kama vile ninavyotaka muwe. Na pia nina wasiwasi kuwa sitakuwa kwa namna ile mnayotaka mimi niwe. Nina hofu kuwa nitawakuta mkibishana, wenye wivu, wenye hasira, mkipigana kwa ubinafsi wenu, wenye misemo mibaya, watetaji, wenye kiburi, na machafuko huko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyano, kunong'ona, majivuno na fujo kati yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyo, kunong'ona, majivuno na fujo kati yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa nina hofu ya kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naogopa, huenda nitakapokuja kwenu nitawakuta katika hali nisiyopenda, nami itanilazimu kuwa katika hali msiyoipenda. Naogopa huenda kukawa na ugomvi, wivu, uhasama, ubishi, masengenyo, kunongona, majivuno na fujo kati yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana naogopa, ya kuwa nitakapokuja sitawaona ninyi, kama nitakavyo kuwaona, tena ya kuwa nami hamtaniona nanyi, kama mtakavyo kuniona. Naogopa kukuta magombano na wivu na mifundo ya mioyo na machokozi na masingizio na mateto na majivuno na matukutiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong’onezo, na majivuno, na ghasia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana ninaogopa kwamba wakati ninapokuja kwenu, sitawakuta sawa vile ninavyotaka, nanyi hamutanikuta sawa vile munavyotaka. Ninaogopa kuwakuta katika fitina, wivu, kasirani, ugomvi, masingiziano, matetano, majivuno na fujo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;