2 Corinthians 12:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi mbeleni, na wala hawajatubu kwa uchafu wao, uasherati, na ufisadi walioushiriki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nina wasiwasi kuwa nitakapokuja kwenu, Mungu wangu ataninyenyekeza tena mbele yenu. Nitalazimika kuomboleza kwa ajili ya wale ambao wametenda dhambi. Wengi wao hawajarejea na kutubia maisha yao ya uovu, dhambi za zinaa, na mambo ya aibu waliyotenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujutia huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi huko nyuma na wala hawajatubia uchafu wao, yaani, uasherati na ufisadi walioufanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi mbeleni, na wala hawajatubu kwa uchafu wao, uasherati, na ufisadi walioushiriki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na uovu walioufanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naogopa huenda hapo nitakapokuja safari ijayo Mungu wangu atanifanya niaibike mbele yenu, nami nitaomboleza kwa ajili ya wengi wa wale waliotenda dhambi lakini hawakujuta huo uchafu, tamaa zao mbaya na uzinzi waliokuwa wamefanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo naogopa kwamba: Nitakapofika kwenu, Mungu wangu ataninyenyekeza tena, nami nitapata kusikitika kwa ajili yao wengi waliokosa kale pasipo kuyajutia mambo ya uchafu na ya ugoni na ya uasherati, waliyoyafanyiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufany
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaogopa kwamba kwa safari yangu ingine, Mungu wangu atanifanya tena kuwa mwenye haya mbele yenu. Nami nitalia kwa ajili ya watu wengi waliofanya zambi zamani nao hawakugeuka toka katika uasherati, uzinzi na tamaa mbaya walizofanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nami nitakapokuja tena, Mungu wangu akanidhili kwenu, nikawasikitikia wengi waliokosa zamani, wala hawakutubia nchafu, na uzinzi, na uasharati walioufanya.