2 Corinthians 12:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nitajivunia juu ya mtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimi binafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitajisifu kwa ajili ya mtu kama huyo, lakini sitajisifu mwenyewe, ila nitajisifia udhaifu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nitajivunia mtu wa namna hiyo, lakini sitajivuna juu yangu mwenyewe. Nitajivuna tu katika madhaifu yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nitajivunia juu ya mtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimi binafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nitajivunia juu ya mtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimi binafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitajisifu kwa ajili ya mtu kama huyo, lakini sitajisifu kuhusu mimi mwenyewe ila mimi nitajisifia udhaifu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitajisifu kwa ajili ya mtu kama huyo, lakini sitajisifu kuhusu mimi mwenyewe ila mimi nitajisifia udhaifu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa kuhusu udhaifu wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nitajivunia juu ya mtu wa namna hiyo, na si juu yangu mimi binafsi, isipokuwa tu juu ya udhaifu wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili yake yeye nitajivuna, lakini kwa ajili yangu mimi hakuna, nitakalojivunia, isipokuwa unyonge wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, nitajivuna kwa ajili ya mutu sawa na yule, lakini sitajivuna kwa ajili yangu mimi mwenyewe, isipokuwa tu kwa ajili ya uzaifu wangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa khabari za mtu huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika khabari ya udhaifu wangu.