2 Corinthians 12:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ningetaka kujivuna singekuwa mpumbavu hata kidogo, maana ningekuwa nasema ukweli tupu. Lakini sitajivuna; sipendi mtu anifikirie zaidi ya vile anavyoona na kusikia kutoka kwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata kama ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga, kwa maana nitakuwa nasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu yeyote asije akaniona mimi kuwa bora kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa nilitaka kujivuna, sitakuwa nikizungumza kama mjinga, kwa sababu ningekuwa nasema iliyo kweli. Lakini sitajivuna tena zaidi, kwa sababu sitaki watu wanifikirie kwa ubora zaidi kuliko wanavyoniona nikitenda ama kusikia ninayosema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama ningetaka kujivuna singekuwa mpumbavu hata kidogo, maana ningekuwa nasema ukweli mtupu. Lakini sitajivuna; sipendi mtu anifikirie zaidi ya vile anavyoona na kusikia kutoka kwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ningetaka kujivuna singekuwa mpumbavu hata kidogo, maana ningekuwa nasema ukweli tupu. Lakini sitajivuna; sipendi mtu anifikirie zaidi ya vile anavyoona na kusikia kutoka kwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata kama ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga, kwa maana nitakuwa nasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu ye yote asije akaniona mimi kuwa bora zaidi kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata kama ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga, kwa maana nitakuwa nasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu yeyote asije akaniona mimi kuwa bora zaidi kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ningetaka kujivuna singekuwa mpumbavu hata kidogo, maana ningekuwa nasema ukweli tupu. Lakini sitajivuna; sipendi mtu anifikirie zaidi ya vile anavyoona na kusikia kutoka kwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ningetaka kujivuna, singekuwa mpuzi, kwani ningesema yaliyo ya kweli. Lakini najikinga, mtu asiniwazie kuwa mkuu kuliko hapo, anionapo na kunisikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ningetaka kujivuna, singekuwa mupumbafu, maana ningesema tu ukweli. Lakini ninaepuka kujivuna, kusudi watu wasinihesabu kuwa mukubwa kuliko vile wanavyoona nikifanya au kunisikia nikisema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini nitajizuia, mtu asinihesabie zaidi ya haya ayaonayo kwangu au kuyasikiakwa kinywa changu.