2 Corinthians 12:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga, nisijivune kupita kiasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
au kwa sababu ya mafunuo haya makuu. Ili kunizuia nisijivune, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini imenipasa kutojivuna zaidi juu ya mambo ya ajabu yaliyoonyeshwa kwangu. Kwa sababu hiyo nilipewa tatizo lenye maumivu; malaika toka kwa Shetani; aliyetumwa kwangu kunitesa, ili nisiweze kufikiri kwamba mimi ni bora zaidi kuliko watu wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga nisijivune kupita kiasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga, nisijivune kupita kiasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ili kunizuia nisijivune kwa sababu ya ufunuo huu mkuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ili kunizuia nisijivune kwa sababu ya ufunuo huu mkuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga, nisijivune kupita kiasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena yako mafunuo makuu yote, niliyoyapata; lakini kwa kwamba nisijikweze kwa ajili yao, nimetiwa chomeo mwilini mwangu, ndio mjumbe wake Satani; akafunguliwa, anipige makonde nisijikweze.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, kusudi nisijivune kupita kipimo kwa ajili ya kupokea ufunuo wa ajabu, nilitiwa katika mwili wangu kitu kinachoniumiza kama mwiba. Kitu kile ni kama mujumbe wa Shetani kwa kunipiga na kunizuiza nisijivune kupita kipimo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kwa sababu ya wingi wa mafunuo hayo, kwa sababu hiyo, nisipate kujivuna kupita kiasi, nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani illi anipige, nisije mkajivuna kupita kiasi.