2 Corinthians 13:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. “Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii itakuwa mara ya tatu mimi kuja kwenu. “Shtaka lolote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuwatembelea. Na mkumbuke, “Kila shitaka ni lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu wanaosema kuwa jambo hilo ni la kweli.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. “Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. “Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo mara ya tatu nikija kwenu. “Shtaka lo lote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ndiyo mara ya tatu mimi kuja kwenu. “Shtaka lolote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hii ndiyo mara yangu ya tatu kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hii ni mara yangu ya tatu kuja kwenu. “Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii itakuwa mara ya tatu, nikija kwenu. Hapo kila jambo litamalizika kwa kusemewa na mashahidi wawili au watatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ni safari yangu ya tatu ninayotayarisha kuja kwenu. Kama Maandiko Matakatifu yanavyosema: “Kila neno linapaswa kuhakikishwa kwa ushuhuda wa watu wawili au watatu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HII ndio marra ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu killa neno litathubutishwa.