2 Corinthians 13:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ndiyo sababu nawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana Isa aliyonipa ya kuwajenga ninyi wala si ya kuwabomoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo, naandika haya nisipokuwapo, ili, nikiwapo, nisiutumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninaandika haya kabla sijaja kwa kuwa niko mbali nanyi ili nijapo nisilazimike kutumia mamlaka kuwaadhibu. Bwana alinipa mamlaka hayo kuwaimarisha, na sio kuwaharibu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ndiyo sababu ninawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana aliyonipa ya kuwajenga ninyi wala si ya kuwabomoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ndiyo sababu nawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana Isa aliyonipa ya kuwajenga ninyi, wala si ya kuwabomoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nisipokuwako kwenu, nayaandikia haya kwamba: Nitakapokuwako kwenu nisitumie ukali wa kukata maneno; nguvu ya kuvifanya hivyo nimepewa na Bwana, lakini ni ya kujenga, siyo ya kujengua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo, naandika haya nisipokuwapo, ili, nikiwapo, nisiutumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa hiyo ninawaandikia maneno haya nikiwa mbali nanyi, kusudi wakati nitakapokuwa kati yenu nisitende kwa ukali kadiri ya mamlaka Bwana aliyonipa. Kwa maana uwezo ule ni kwa ajili ya kuwajenga katika imani, lakini si wa kubomoa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa biyo, naandika liayo nisipokuwapo, illi, nikiwapo, nisitumie ukali kwa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana illi kujenga wala si kubomoa.