2 Corinthians 13:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, farijianeni, kuweni na nia moja, na mkae kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa, wapendwa dada zangu na kaka zangu mjazwe furaha. Jitahidini kutengeneza njia zenu, fanyeni nilichowaomba kufanya. Mpatane kila mmoja na mwenziwe, na ishini katika amani. Ndipo Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa mapendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Iweni wakamilifu, mkafarijike, nieni pamoja, kaeni kwa amani, naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwisho, ndugu, furahini, mtengenezane, mwonyane, mioyo yenu iwe mmoja, mpate kutengemana! Ndipo, Mungu aliye mwenye upendo na matengemano atakapokuwa pamoja nanyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kwa kumaliza, wandugu zangu, kwa heri. Mujikaze kuwa wakamilifu, mufarijiane ninyi kwa ninyi, mukuwe na nia moja, muishi katika amani, na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.