2 Corinthians 13:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tena nikiwa mbali: Wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja, sitakuwa na huruma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliwaonya nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili. Sasa narudia wakati sipo, kwamba nikija tena sitawahurumia wale waliokuwa wametenda dhambi hapo awali au wengine wote,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili, nilitoa maonyo kwa wale waliotenda dhambi. Sipo hapo sasa, ila natoa onyo lingine kwao na kwa yeyote aliyetenda dhambi: Nitakapo kuja tena kwenu, nitawaadhibu walio miongoni mwenu ambao bado wanatenda dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tena nikiwa mbali: wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja, watakiona cha mtema kuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tena nikiwa mbali: wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja, sitakuwa na huruma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekwisha kuwaonya nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili. Sasa narudia wakati sipo, kwamba nikija tena sitawahurumia wale waliokuwa wametenda dhambi hapo awali na wengine wote,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekwisha kuwaonya nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili. Sasa narudia wakati sipo, kwamba nikija tena sitawahurumia wale waliokuwa wametenda dhambi hapo awali na wengine wote,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilikwisha sema, na kama ilivyokuwa safari ya pili, sasa nasema tena nikiwa mbali: Wale wote waliotenda uovu bila kutubu, na pia wale wengine, nitakapokuja, sitakuwa na huruma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimekwisha kusema kale, nilipokuwako kwenu mara ya pili, tena nayasema sasa, nisipokuwako kwenu, kwamba: Waliokosa kale nao wote wengine, hapo, nitakapokuja tena sitawapatia upole.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa wakati huu ninapokuwa mbali nanyi, ninarudilia kuwaambia waziwazi maneno yale niliyokuwa nimekwisha kuwaambia mbele katika safari yangu ya pili niliyofanya kwenu. Ninawaambia kwamba nitakapokuja kwenu mara tena, sitakosa kuazibu wale waliofanya zambi zamani na wengine wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nimetangulia kuwaambia: na kama vile nilipokuwapo marra ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo natangulia kuwaambia wao waliofanya dhambi zamani, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia: