2 Corinthians 13:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa mnadai uthibitisho kwamba Al-Masihi anazungumza kwa kunitumia mimi. Yeye si dhaifu katika kushughulika nanyi, bali ana nguvu kati yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnatafuta uthibitisho kuwa Kristo anasema kupitia mimi. Uthibitisho wangu ni kuwa yeye si dhaifu kuwashughulikia bali yeye anaonesha uweza wake miongoni mwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa mnadai uthibitisho kwamba Kristo anazungumza kwa kunitumia mimi. Yeye si dhaifu katika kushughulika nanyi, bali ana nguvu katikati yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa mnadai uthibitisho kwamba Al-Masihi anazungumza kwa kunitumia mimi. Yeye si dhaifu katika kushughulika nanyi, bali ana nguvu kati yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtajionea wenyewe kwamba Kristo anasema ndani yangu. Kwenu Kristo si dhaifu; bali nguvu yake yafanya kazi miongoni mwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mwataka kujaribu, kama ni Kristo kweli anayesema kinyuwani mwangu; naye hawaendei kwa unyonge, ila hutenda nguvu kwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitafanya vile kwa sababu ninyi munataka uhakikisho kwamba Kristo anasema kwa njia yangu. Kwenu Kristo si zaifu, lakini anaonyesha uwezo wake kati yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemae ndani yangu, ambae si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu.