2 Corinthians 13:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jichunguzeni nyinyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani. Jichunguzeni nyinyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi nyinyi mmeshindwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Isa Al-Masihi yu ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jiangalieni ninyi wenyewe. Mjipime ninyi wenyewe mkaone kama mngali mnaishi katika imani. Hamtambui kuwa Kristo Yesu yu ndani yenu? La mkishindwa jaribio hilo; ikiwa hamtakuwa mkiishi katika imani; basi Kristo hayumo ndani yenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jichunguzeni ninyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani. Jichunguzeni ninyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi ninyi mmeshindwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jichunguzeni nyinyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani. Jichunguzeni nyinyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi nyinyi mmeshindwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Yesu Kristo yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Isa Al-Masihi yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jichunguzeni nyinyi wenyewe mpate kujua kama kweli mnayo imani. Jichunguzeni nyinyi wenyewe. Je, hamjui kwamba Kristo Yesu yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi nyinyi mmeshindwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jijaribuni, kama mnakuwa mnamtegemea! Jionyesheni kuwa wakweli! Au hamjitambui wenyewe, kama Yesu Kristo mnaye mwenu? Msipoyajua, ham wa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mujichunguze ninyi wenyewe kusudi mupate kujua kama munasimama imara katika imani. Mujipime. Si munajua kwamba Yesu Kristo anakaa kati yenu? Kama si vile ni kusema kwamba mumeshindwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jijaribuni nafsi zenu kwamba m katika imani; jithubutisheni nafsi zenu. Au bamjijui nafsi zenu, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu isipokuwa mmekataliwa?