2 Corinthians 13:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi tunaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi twamwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, tujapokuwa sisi tu kama waliokataliwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunawaombea kwa Mungu msifanye lolote lililo baya. Tunachojali hapa si kwamba watu waone kuwa tumeshinda jaribio katika ile kazi tuliyofanya pamoja nanyi. Tunachokitaka zaidi ni ninyi kufanya lililo jema, hata ikiwa itaonekana kuwa tumeshindwa jaribio.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi tunaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi tunaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lo lote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi tunamwomba Mungu, msifanye lolote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, ijapokuwa sisi tu kama waliokataliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunamwomba Mungu msifanye uovu wowote, lakini si kusudi tuonekane kama watu waliokwisha faulu, bali mpate kutenda mema, hata kama sisi tunaonekana kuwa tumeshindwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini twamwomba Mungu, ninyi msifanye uovu wo wote, siko kwamba sisi tuonekane kuwa wakweli, ila ni kwamba ninyi myafanye yaliyo mazuri, nasi tuwe kama waongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi twamwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, tujapokuwa sisi tu kama waliokataliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nasi tunaomba Mungu kusudi musifanye jambo lolote baya, nasi hatutaki kuonyesha kwamba tumeshinda. Lakini tunataka mutende mema hata ikionekana kuwa sisi tunashindwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na namwomba Mungu, msifanye lo lote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, bali ninyi mfanye lililo jema, tujapokuwa sisi kama waliokataliwa.