2 Corinthians 2:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Al-Masihi kwa ajili yenu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mkimsamehe mtu, ndipo nami husamehe pia. Na kile nilichosamehe, kama nilikuwa na jambo la kusamehe, nilisamehe kwa ajili yenu. Na Kristo akithibitisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe—kama kweli ninacho cha kusamehe—nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ninyi mkimsamehe mtu ye yote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu cho chote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Al-Masihi kwa ajili yenu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama mkimsamehe mtu neno lolote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lolote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mmwachiliaye neno, hata mimi humwachilia. Kwamba hata mimi, ikiwa nimemwachilia mtu neno, nimemwachilia kwa ajili yenu machoni pa Kristo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati munaposamehe mutu, nami ninamusamehe vilevile. Kwa maana kama ninasamehe, na ikiwa kweli ninakuwa na neno lolote la kusamehe, ninasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo,