2 Corinthians 2:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mungu apewe shukrani, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Al-Masihi. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ashukuriwe Mungu ambaye siku zote hutuongoza katika gwaride la ushindi la Kristo. Mungu anatutumia sisi kueneza ufahamu juu ya Kristo kila mahali kama vile marashi yanayonukia vizuri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye kwa kupitia sisi hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mwenyezi Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Al-Masihi. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mungu atukuzwe anayetupa kushinda siku zote, tukiwa katika Kristo! Kwa hivyo, tunavyomtumikia yeye, hutokeza po pote waziwazi, ya kuwa wenye kumtambua wafanana na maua yanukayo vizuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Mungu ashukuriwe, maana yeye ndiye anayetupatia ushindi siku zote katika ushirika wetu pamoja na Kristo. Anatutumia sisi kwa kutambulisha Kristo pahali pote kama vile harufu nzuri ya marasi inavyosambaa popote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.