2 Corinthians 2:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na neno la Mungu ili tujifaidishe. Bali tunalinena neno lake kwa unyofu katika Al-Masihi tukiwa mbele za Mungu, kama watu waliotumwa na Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hakika sio wale wanaozunguka wakiuuza ujumbe wa Mungu ili kupata faida! Lakini sisi hatufanyi hivyo. Kwa msaada wa Kristo tunaisema kweli ya Mungu kwa uaminifu, tukifahamu kuwa tunazungumza kwa ajili yake na mbele zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Kristo tunalisema Neno la Mungu kwa unyofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Al-Masihi tunalisema Neno la Mungu kwa unyoofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana sisi si kama walio wengi, walichuuzao neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sisi hatufanani nao wale wengi wanaolichuuzia Neno la Mungu, ila kwa ung'avu wa mioyo, tulioupata kwa Mungu, tunasema kama watu walio pamoja na Kristo mbele yake Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi sisi si kama wengine wengi wanaochuuza neno la Mungu; lakini kwa sababu Mungu ndiye aliyetutuma, sisi tunasema ukweli mbele yake, kama vile watumishi wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.