2 Corinthians 2:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi, ila amewahuzunisha nyinyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa mtu yeyote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote. Nasema hivi ili nisiwe mkali kupita kiasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu mmoja katika kusanyiko lenu amesababisha maumivu, ila si kwangu, bali amesababisha maumivu kwenu nyote kwa kiwango fulani. Nina maanisha amewakwaza nyote kwa namna fulani. (Sitaki ionekane kuwa mbaya sana kuliko ilivyo)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi—ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi, ila amewahuzunisha nyinyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa mtu ye yote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote, ili nisiwe mkali kupita kiasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa mtu yeyote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote, ili nisiwe mkali kupita kiasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi, ila amewahuzunisha nyinyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama yuko aliyesikitisha, hakunisikitisha mimi; ila fungufungu, maana nisiseme na kuyapita ya kweli, amewasikitisha ninyi nyote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa mutu aliyefanya mambo ya kuhuzunisha, hakunihuzunisha mimi, lakini amewahuzunisha ninyi wote au bila kwenda mbali zaidi wamoja kati yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi, bali kwa sehemu ninyi nyote, nisije nikawalemea.