2 Corinthians 3:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu, kikilinganishwa na huu utukufu unaozidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Utaratibu wa zamani wa utumishi kwa Mungu ulikuwa na utukufu. Lakini kwa hakika unapoteza utukufu wake unapolinganishwa na utukufu mkubwa zaidi wa utaratibu mpya wa utumishi kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu uzidio sana wa Agano Jipya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu unaozidi wa Injili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani utukufu ule uliokuwa wa kifungufungu tu tukiufananisha na utukufu huu uzidio kabisa tutasema: Ule sio utukufu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunaweza kusema kwamba ule utukufu uliongaa zamani hauwezi kulinganishwa na utukufu wa sasa unaokuwa mukubwa zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana hatta ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu kwa sababu hii, kwa ajili ya utukufu uzidio sana.