2 Corinthians 3:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa utumishi ule wa muda ulikuja na utukufu, basi utumishi wa kudumu umekuja na utukufu mkubwa zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, si zaidi sana utukufu wa kile kinachodumu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile idumuyo ina utukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani chenye kutoweka kikiwa na utukufu, chenye kuwapo kitakuwa na utukufu uupitao ule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kama mambo yaliyokuwa ya muda tu yalipata utukufu, basi yale yanayodumu ni yenye utukufu zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu ukomao, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu udumuo.