2 Corinthians 3:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mngao ule uliokuwa unafifia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sisi si kama Musa, ambaye ilimpasa kuweka utaji wa kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng’ao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hatuko kama Musa, ambaye alifunika uso wake ili watu wa Israel wasiendelee kuona kuwa utaratibu wa zamani wa kumtumikia Mungu ulikuwa unaelekea mwisho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mng'ao uliokuwa unafifia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mng'ao ule uliokuwa unafifia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng'ao uliokuwa juu yake wakati ukififia na hatimaye kutoweka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sisi si kama Musa, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng’ao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mngao ule uliokuwa unafifia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nasi hatufanyi kama Mose aliyeufunika uso wake kwa mharuma, wana wa Isiraeli wasipate kuutazama mwisho wa yale yaliyo yenye kutoweka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi hatufanyi kama Musa alivyokuwa akifunika uso wake na kitambaa kwa kuzuiza Waisraeli wasiangalie mwisho wa utukufu uliokuwa wa muda tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, illi wana wa Israeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;