2 Corinthians 3:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana hadi leo utaji ule ule hufunika Torati inaposomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Al-Masihi peke yake unaondolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mioyo yao ilikuwa imefungwa. Na hata leo, watu wale wanapolisoma agano la kale, fahamu zao zinakuwa zimefunikwa. Ni kwa kupitia Yesu Kristo tu agano la kale linaondolewa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale lisomwapo. Huo utaji haujaondolewa kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Torati inasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Al-Masihi peke yake unaondolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji huo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mawazo yao yakashupazwa. Kwani mpaka siku ya leo wakilisoma Agano la Kale, liko limefunikwa vivyo hivyo, lisiwafunukie kwamba: Limetimilia katika Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini akili yao ilikuwa nzito kwa kufahamu. Kwa maana mpaka sasa, Waisraeli wanaposoma katika vitabu vya Agano la Kale, akili yao inafunikwa na kitambaa kile kile. Kitambaa kile kitaondolewa tu kwa mutu anayeungana na Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo;