2 Corinthians 3:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, unaotoka kwa Bwana Isa, aliye Roho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na sura zetu hazikufunikwa. Sote tunaendelea kuutazama utukufu wa Bwana, na tunabadilishwa na kufanana na mfano huo huo tunaouona. Badiliko hili linatuletea utukufu zaidi na zaidi, na linatoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, twaonyesha kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana Isa, ambaye ndiye Roho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano huo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nasi sote tunautazama utukufu wa Bwana kwa macho yasiyofunikwa, kama twauona katika kioo; ndivyo, tunavyogeuzwa, tufanane naye, tukipewa utukufu kwa utukufu, tuwe kama watu waliogeuzwa na Bwana mwenyewe aliye Roho.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi wote ambao uso haukufunikwa, tunaonyesha kama kioo utukufu wa Bwana. Kwa hiyo, tunabadilishwa kwa kufanana na Bwana, nasi tunapita toka utukufu mumoja hata utukufu mwingine unaokuwa mukubwa zaidi tena. Kwa maana kazi hii inatimizwa na Bwana ndiye Roho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.