2 Corinthians 3:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simaanishi kuwa tuna uwezo wa kufanya jambo lolote jema kwa uwezo wetu wenyewe. Mungu ndiye anatuwezesha kufanya yote tunayoyafanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lo lote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Si kwamba tunatosha sisi wenyewe kufikiri kuwa neno lolote ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huku siko kwamba: Twafaa kuwaza neno lo lote kwa kulitoa mioyoni mwetu; kama liko, tuliwezalo, tutagawiwa na Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Si kusema kwamba sisi wenyewe tuko na uwezo wa kujitungia jambo hili, lakini uwezo wetu unatoka kwa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu,