2 Corinthians 3:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si agano la sheria iliyoandikwa, bali agano la Roho. Maana sheria iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uhai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndiye alitutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho wa Mungu; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ametuwezesha pia kuwa watumishi wa agano jipya lililotoka kwake kwenda kwa watu wake. Si agano la sheria zilizoandikwa, ni la Roho. Sheria zilizoandikwa huleta mauti, bali Roho huleta uzima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si agano la sheria iliyoandikwa, bali Agano la Roho. Maana sheria iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uzima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si agano la sheria iliyoandikwa, bali agano la Roho. Maana sheria iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uhai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye ndiye aliyetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si agano la sheria iliyoandikwa, bali agano la Roho. Maana sheria iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uhai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye ndiye aliyetupa kuwa watumishi wafaao wa Agano Jipya lisilo la andiko, ila la Roho. Kwani andiko huua, lakini Roho hutupatia uzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Mungu ndiye aliyetuwezesha kuwa watumishi wa agano jipya, lisilotokana na Sheria iliyoandikwa, lakini na Roho. Sheria iliyoandikwa inaleta kifo lakini Roho analeta uzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.