2 Corinthians 3:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mngao wake. Tena mngao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe, ilikuja kwa utukufu hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Musa kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa wa kufifia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Agano la kale lililoleta mauti, lililoandikwa kwenye mawe, lilikuja na utukufu wa Mungu. Kwa kweli, uso wa Musa ulikuwa unang'aa utukufu (Utukufu uliokuwa na ukomo) hata watu wa Israel hawakuweza kuendelea kumtazama usoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mng'ao wake. Tena mng'ao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mng'ao wake. Tena mng'ao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, ile iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa ni wa kufifia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu, hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Musa kwa sababu ya ule utukufu wake ingawa ulikuwa ni wa kufifia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mngao wake. Tena mngao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao utumishi wa mambo yenye kuua, yaliyokuwa yameandikwa na kuchorwa maweni, ulikuwa na utukufu wake, ukawazuia wana wa Isiraeli kuutazama uso wake Mose kwa ajili ya utukufu wa uso wake uliokuwa wa kutoweka tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sheria ile inayoleta kifo imeandikwa neno kwa neno juu ya vibao vya mawe na utukufu wa Mungu ulingaa wakati ule. Uso wa Musa ukangaa vilevile hata Waisraeli hawakuweza kuangalia uso wake ingawa kungaa kule kulikuwa kwa muda tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, ikiwa khuduma ya mauti katika maandiko, iliyochorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hatta wana wa Israeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao utukufu uliokuwa ukibatilika;