2 Corinthians 3:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma iletayo uadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maana yangu ni kuwa: utaratibu wa zamani wa kumtumikia Mungu uliwaweka watu katika hatia ya dhambi na kuwapa hukumu, lakini lilikuwa na utukufu. Hivyo kwa hakika utaratibu mpya wa kumtumikia Mungu unaowaweka huru watu kutoka hukumu una utukufu mkubwa zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma ile iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma iletayo uadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa huduma ile iwahukumuyo wanadamu ina utukufu, je, haitakuwa ya utukufu zaidi ile huduma iletayo haki?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, sembuse huduma ya haki ina utukufu unaozidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma iletayo uadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani utumishi utupatiao hukumu ukiwa na utukufu, utumishi utupatiao wongofu utakuwa na utukufu ulio mkuu zaidi kuliko ule.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa utumishi unaowaletea watu hukumu ulikuwa na utukufu, basi si zaidi sana utumishi unaowafanya watu wahesabiwe haki mbele ya Mungu, utakuwa na utukufu mukubwa zaidi?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana ikiwa khuduma ya hukumu ina utukufu, khuduma ya haki ina utukufu unaozidi sana.