2 Corinthians 4:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, muda tuishipo tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uhai wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Isa, ili uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuko hai, lakini kwa ajili ya Yesu tupo katika hatari ya kifo kila wakati, ili kwamba uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ya kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naam, katika maisha yetu yote tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uzima wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, muda tuishipo tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uhai wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Isa, ili kwamba uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, muda tuishipo tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uhai wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sisi tunaoishi hutolewa kila siku, tuuawe kwa ajili ya Yesu kwamba: Nako kuishi kwake Yesu kupate kutokea katika miili yetu iliyo yenye kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana katika maisha yetu, tunakuwa kila mara katika hatari ya kufa kwa ajili ya Yesu, kusudi uzima wake uonekane vilevile katika mwili wetu unaokuwa wa kufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti.