2 Corinthians 4:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yote haya ni kwa faida yenu, hata neema ya Mungu inapowafikia watu wengi zaidi na zaidi, shukrani nazo ziongezeke zaidi, kwa utukufu wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yote ni kwa faida yenu, ili neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mambo yote haya ni kwa ajili yenu. Na hivyo neema ya Mungu inatolewa kwa watu wengi zaidi na zaidi. Hili litaleta shukrani nyingi zaidi na utukufu kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yote haya ni kwa faida yenu; ili kama vile neema ya Mungu inavyoenea kwa watu wengi zaidi na zaidi vivyo hivyo watu wengi zaidi watoe shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yote haya ni kwa faida yenu, hata neema ya Mungu inapowafikia watu wengi zaidi na zaidi, shukrani nazo ziongezeke zaidi, kwa utukufu wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yote haya ni kwa faida yenu, hata neema ya Mungu inapowafikia watu wengi zaidi na zaidi, shukrani nazo ziongezeke zaidi, kwa utukufu wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani yote hutupata kwa ajili yenu, maana wenye kugawiwa kipaji wakiwa wengi, hao wengi nao watakazana kuutukuza utukufu wake Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mambo haya yote yanafika kwa ajili yenu kusudi neema ya Mungu izidishwe kwa watu wengi siku zote, nao wapate kumutolea Mungu shukrani nyingi kwa ajili ya utukufu wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe.