2 Corinthians 5:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapongolewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana twajua kama hema letu la dunia tunayoishi likiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunafahamu kuwa miili yetu, ambayo ni hema tunaloishi ndani yake hapa duniani itaharibiwa. Hilo litakapotokea, Mungu atakuwa na nyumba tayari kwa ajili yetu kuishi ndani yake. Haitakuwa nyumba kama ambayo watu hujenga hapa duniani. Itakuwa nyumba ya mbinguni itakayodumu milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana tunajua kwamba hema hii ambayo ndani yake tunaishi sasa hapa duniani, yaani mwili wetu, itakapong'olewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapong'olewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana twajua kwamba kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana tunajua kwamba hema hii ambamo tunaishi sasa hapa duniani yaani mwili wetu, itakapongolewa, Mungu atatupa makao mengine mbinguni, nyumba ya milele isiyotengenezwa kwa mikono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani twajua, ya kuwa hivi vijumba vyetu, tupangamo nchini, vitakapobomolewa, tunayo majengo yaliyojengwa na Mungu, ni nyumba zisizojengwa na mikono ya watu, nazo hukaa kale na kale huko mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana, tunajua kwamba hema hii tunayoishi ndani yake hapa katika dunia, maana yake mwili wetu, itakapobomolewa, Mungu atatupatia makao mengine mbinguni. Nayo ni nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe na inayodumu milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu.