2 Corinthians 5:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Al-Masihi, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tutasimama sote mbele za Kristo ili tuhukumiwe. Kila mtu atalipwa anachostahili. Kila mtu atalipwa kutokana na matendo yake, mazuri au mabaya, alipoishi katika mwili huu wa kidunia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Al-Masihi, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee malipo ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, yawe ni mema au mabaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sisi sote sharti tutokee mbele ya kiti cha uamuzi cha Kristo, kila mmoja alipwe, aliyoyafanyiza alipokuwa mwilini, yakiwa mema au maovu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana sisi wote tunapaswa kusimama kwa kusambishwa mbele ya tribinali ya Kristo, kusudi kila mutu alipwe kufuatana na matendo yake mema au mabaya aliyofanya alipokuwa akiishi ndani ya mwili wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.