2 Corinthians 5:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Al-Masihi kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuanzia sasa hatumfikirii mtu yeyote kama ulimwengu unavyowafikiria watu. Ni kweli kuwa zamani kale tulimfikiria Kristo kwa mtazamo wa kidunia. Lakini hatufikirii hivyo sasa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu ye yote kwa mtazamo wa kibinadamu, ingawa wakati fulani tulimwangalia Kristo kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena kwa jinsi hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Al-Masihi kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo tangu sasa hakuna, tunayemjua kimwili. Ikiwa tulimtambua Kristo kimwili, sasa hatumtambui tena hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo basi, tangu sasa hatumuhesabu tena mutu yeyote kufuatana na hali ya kimutu. Hata ikiwa tulimuhesabu Kristo kufuatana na hali ya kimutu, kwa sasa hatumuhesabu tena kufuatana na hali ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena.