2 Corinthians 5:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu anapokuwa ndani ya Kristo, anakuwa kiumbe kipya kabisa. Mambo ya zamani yanakoma; na ghafla kila kitu kinakuwa kipya!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo mtu akiwa anaye Kristo, amekuwa kiumbe kipya. Yake ya kale yamepita; ukimtazama, yote yamekuwa mapya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mutu yeyote anapoungana na Kristo, yeye anakuwa kiumbe kipya. Mambo ya zamani yametoweka, na sasa hali mupya imefika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.