2 Corinthians 5:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kupitia kwa Isa Al-Masihi, na kutupatia sisi huduma ya upatanisho:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yote haya yatoka kwa Mungu. Kupitia Kristo, Mungu alifanya amani katika yake na sisi. Na Mungu alitupa kazi ya kuleta amani kati ya watu na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, akatupa nasi jukumu la kuwapatanisha watu naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupatia sisi huduma ya upatanisho:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yote yanatokana na Mwenyezi Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Isa Al-Masihi na kutupata sisi huduma ya upatanisho:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yote ni kazi ya Mungu mwenye kutupatanisha sisi naye kwa njia ya Kristo, na kutupa jukumu la kuwapatanisha watu naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo yote hutoka kwa Mungu; ndiye aliyetupatanisha sisi naye yeye, Kristo alipojitoa. Kisha akatupa kuyatumikia hayo mapatano
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo haya yote yalifanyika na Mungu, aliyetupatanisha naye kwa njia ya Kristo na kutupatia kazi ya kuongoza watu wengine wapatane naye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho;