2 Corinthians 5:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi nyinyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Al-Masihi, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Al-Masihi: mpatanishwe na Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo tumetumwa kwa ajili ya Kristo. Ni kama Mungu anawaita watu kupitia sisi. Tunazungumza kwa niaba ya Kristo tunapowasihi ninyi kuwa na amani na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi ninyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi nyinyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa vyetu, nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Al-Masihi, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Al-Masihi, mpatanishwe na Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sisi tunamwakilisha Kristo, naye Mungu mwenyewe anatutumia sisi kuwasihi nyinyi. Tunawaombeni kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo sisi tu wajumbe mahali pake Kristo; ndivyo Mungu mwenyewe anavyowaonya kwa vinywa vyetu sisi. Maana twawabembeleza mahali pa Kristo: Yapokeeni hayo mapatano yake Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi sisi ni wajumbe wa Kristo. Kwa njia yetu, Mungu mwenyewe anawaita ninyi; na kwa hiyo tunawasihi katika jina la Kristo, mukubali kupatanishwa na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anakusihini kwa vinywa vyetu: twawaombeni kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.