2 Corinthians 6:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuna huzuni nyingi, lakini tunafuraha kila siku. Tu maskini, lakini tunawafanya watu wengi kuwa matajiri katika imani. Hatuna kitu, lakini tunakila kitu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini hohehahe, lakini twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama wenye huzuni lakini siku zote tukifurahi, tukionekana maskini lakini tukitajirisha wengi, tukiwa kama wasio na kitu lakini tuna vitu vyote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini, twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tuko kama wenye kusikitika, lakini twafurahi po pote; tuko kama maskini, lakini twagawia wengi mali nyingi; tuko kama wasio na kitu cho chote, lakini vyote tunavyo.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tunahuzunishwa lakini tunafurahi siku zote. Tunaonekana kama wamasikini lakini tunatajirisha watu wengi, hatuna kitu, lakini tunakuwa na vitu vyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.